Mwigizaji Mkongwe wa Filamu Nchini, Issa Joseph maarufu kama Mzee Onyango amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 11, 2026 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mtoto wa marehemu, Joshua Joseph Issa amesema Baba yake alikuwa akiugua kwa muda na umauti ulimkuta majira ya saa 8 usiku akiwa Hospitalini hapo.
Pia amesema kuwa familia bado inaendelea na vikao vya maandalizi ya mazishi na kwamba taarifa rasmi kuhusu ratiba na taratibu za mazishi zitatolewa baadaye kwa umma.
Kwa upande wake, Rafiki wa karibu wa marehemu na Mwigizaji mwenzake wa muda mrefu, Mahamood Marijebi maarufu kama Mwita Mwaranya, amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho.
Msiba wa Mzee Onyango upo Kawe jirani na Viwanja vya Gofu vya Lugalo,
