Wakulima wa zao la parachichi wilayani Ngara Mkoani Kagera wametakiwa kulima kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kilimo ili kuendana na hali ya soko lililopo kwa sasa.
Ushauri huo umwtolewa na Afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw. Gudluck Leonard wakati akizungumza na radio kwizera ofisini kwake namna wakulima wanavyoweza kunufaika na zao hilo.
Bw. Laonard amesema Idara ya Kilimo wanaendelea kuweka mikakati ya kutoa elimu ya uvunaji kwa mkulima ili anufaike na zao hilo ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha na wanunuzi wa zao hilo.
Baadhi ya wakulima wa Parachcihi wamewaomba maafisa kilimo kuendelea kutoa elimu ya soko la parachichi kuepukana na walanguzi wanaomhujumu mkulima kwa vipimo ili kuongeza tija zaidi.
