Na Amos John- Shinyanga.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaendelea kuweka kipaumbele katika kuboresha mazingira ya kujifunzia katika taasisi za elimu ya juu nchini ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu katika mazingira bora.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo leo Jumatatu, Novemba 9, 2026, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya elimu ya juu katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, iliyopo mkoani Shinyanga.

Akiwa chuoni hapo, Waziri Mkuu amengumza na wanafunzi na viongozi wa chuo hicho baada ya kukagua miundombinu hiyo, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuhakikisha mazingira ya kujifunzia yanaboreshwa, huku akiwataka wanafunzi kuweka jitihada katika masomo yao na kutumia fursa zilizopo kusonga mbele kielimu.
Akizungumzia ziara hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema Waziri Mkuu amefika chuoni hapo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi na kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi, na si kwa ajili ya kuzindua majengo hayo au kuweka jiwe la msingi.

