Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Antoine Tshisekedi, amemtunuku mwanamuziki maarufu Fally Ipupa nishani ya heshima ya kitaifa, ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika kuitangaza nchi hiyo kupitia muziki.
Heshima hiyo imetolewa kufuatia mafanikio ya kihistoria ya Fally Ipupa kufanya tamasha kubwa katika Uwanja wa Stade de France, ambapo ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Mwafrika anayezungumza Kifaransa na anayeishi barani Afrika kutumbuiza katika uwanja huo maarufu.
Akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo hiyo, Rais Tshisekedi alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuthamini kipaji, nidhamu, uvumilivu na mchango wa msanii huyo katika kueneza utamaduni wa Congo katika jukwaa la kimataifa.
Fally Ipupa anaendelea kuwa mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, akitumia muziki wake kuiwakilisha DR Congo duniani.
