Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya na UNCDF imeweka mikakati ya kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kufikia asilimia 80 ya kaya ifikapo mwaka 2034.
Akizungumza katika kongamano la nishati safi jijini Arusha, Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema serikali inalenga kufanikisha hilo kupitia maboresho ya sera, uwekezaji na elimu kwa umma.
Kwa upande wake, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Christine Grau, amesema EU imetenga euro milioni 30 kusaidia upanuzi wa huduma za nishati safi.
Naye Mshauri Mkuu wa Kiufundi wa UNCDF, Peter Malika, amesema zaidi ya kaya 413,000 tayari zimenufaika kupitia programu ya CookFund.
