Convert to PDF
Wakulima mkoani Singida wametakiwa kuhakiki uhalisi wa mbegu za mahindi na kuchagua aina zinazolingana na mazingira ya mashamba yao ili kupunguza hatari ya uzalishaji na kulinda uwekezaji wao katika kilimo.
Uhamasishaji huo unakuja wakati Tanzania ikiendelea na juhudi za kuongeza uzalishaji wa mahindi kupitia Ajenda 10/30, inayolenga kufikia wastani wa tani sita kwa hekta ifikapo mwaka 2030.
Msimamizi wa Mauzo wa Bayer Life Science Tanzania, Edilitruda Temba amesema elimu kuhusu ubora wa mbegu na uchaguzi wa aina zinazofaa ni muhimu katika kuwasaidia wakulima kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuanza kwa msimu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya miezi minne ya DEKALB Mafanikio Shambani, amesema wakulima wanaweza kuhakiki mbegu zenye kibandiko cha kielektroniki cha TOSCI kwa kupata namba ya utambulisho na kupiga 14852# kupitia simu zao za mkononi.
Kampeni hiyo, inayoendeshwa na Bayer East Africa kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya mbegu, inatoa elimu kuhusu aina tano za mahindi chotara za DEKALB na uchaguzi wa mbegu kulingana na mazingira ya kilimo, ikiwemo maeneo yenye mvua chache na changamoto za magonjwa.
