Wananchi wa Buchosa, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, wameipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuhakikisha mbolea za kupandia zinawafikia wakulima kwa wakati, huku mvua za msimu wa kilimo zikiwa zimeanza kunyesha.
Wakizungumza kuhusu upatikanaji wa pembejeo hizo, Wananchi wameeleza kuwa hatua hiyo imewapa matumaini ya kuanza shughuli za kilimo kwa wakati na kuongeza uzalishaji wa mazao katika msimu huu.
Mkazi wa Kata ya Kafunzo, Amina John, amempongeza Daniel Chongolo kwa jitihada za kuhakikisha Wakulima wanapata mbolea za kupandia kwa wakati, akisema hatua hiyo itawasaidia kutumia vyema msimu wa mvua na kuongeza nafasi ya kupata mavuno mengi.
Kwa upande wake, Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amesema awali kulikuwa na dalili za kuchelewa kwa mbolea, lakini baada ya kuwasiliana na Chongolo, hatua zilichukuliwa na kuhakikisha pembejeo hizo zinawafikia Wakulima..
