Mdau mkubwa wa muziki wa Singeli Majizzo amempongeza Samio kwa mchango wake katika kukuza muziki wa Singeli, akimtaka kuendelea kupambana na kuikuza tasnia hiyo licha ya changamoto zinazoweza kujitokeza.
Majizzo amesema kazi ya kuipigania Singeli haina kustafu wala kujitoa, akisisitiza kuwa hata mtu akipigwa mishale, anapaswa kuendelea na safari.
Pia amemtaka Samio kuendelea kushirikiana na wasanii, wadau na wazalishaji wengine katika kukuza muziki huo, huku akimshukuru kwa kazi kubwa aliyoifanya, hasa akiwa na Pacha wake wa Redioni, Fidomgaigai.
Amemuandikia ujumbe huu baada ya Samio kutangaza kustaafu kujihusisha na muziki wa Singeli siku chache zilizopita baada ya kuona amedharauliwa na msanii wa Singeli Kinata Mc,“Samio wa Kienyeji, endelea kuwa wewe, wewe na wanangu wengine Lazima muendelee kuzalisha vipaji vingine na kuupa Muziki hadhi kubwa,”
