Macho na masikio ya wapenzi wa soka ulimwenguni kote leo yatakuwa yameelekezwa katika Jumba la Maonyesho la London Palladium, ambapo washindi wa tuzo mashuhuri za Ballon d’Or 2026 watatangazwa rasmi usiku wa leo.
Hii ni mara ya kwanza katika historia kwa sherehe hizi kubwa za utoaji wa tuzo hizo kufanyika nje ya nchi ya Ufaransa, hatua inayoongeza msisimko wa kipekee katika tasnia ya soka.

Sherehe hizo za awamu ya 70 zitahudhuriwa na magwiji wa soka, makocha, na watu mashuhuri, huku zikiendeshwa na mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa, Thierry Henry, akishirikiana na mtangazaji mahiri Kate Scott.
Tofauti na miaka ya nyuma, msimu huu unatajwa kuwa na ushindani mkali zaidi, huku vigezo vya tuzo hiyo vikizingatia kiwango cha wachezaji kwa msimu mzima wa 2025โ26 (kuanzia Agosti 3, 2025 hadi Julai 19, 2026) badala ya mwaka wa kalenda wa msimu wa soka
Wachambuzi wengi wa soka wanamtaja nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane, kama mchezaji anayepigia upatu mkubwa, wa kushinda tuzo hiyo.
