Chupa 1,795 za dawa tiba zenye asili ya kulevya zimekamatwa ndani ya basi la abiria linalofanya safari zake kati ya Tanzania, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Kamishna Jeneralia wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari leo March 04 2026 Jijini Dar es Salaam amesema kuwa kiwango hicho ni kikubwa zaidi kukamatwa katika miaka ya karibuni.
Kukamatwa kwa dawa hizo ni matokeo ya oparesheni iliyofanywa kati ya maofisa wa forodha mpaka wa Mtukula na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).
Katika Oparesheni hiyo zimekamatwa boksi 105 za Pethidine zenye chupa 1,045, boksi 31 za Morfine Sulphate zenye chupa 310 na boksi 44 za Fentanyl zenye chupa 440.
Dawa hizo zimekamatwa katika basi la Kampuni ya SR Classic kutoka DRC, linalofanya safari zake kati ya Uganda, Tanzania na DRC, wakati likiingia nchini kupitia mpaka wa Mutukula.
