Kiungo wa klabu ya Simba Jospin Loemba amemuomba msamaha beki wa kati wa klabu ya Yanga Dickson Job baada ya kumsababishia majeraha katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Istagram Loemba amemtaka radhi na kuonesha kwamba yupo pamoja nae katika kile anachokipitia kwasasa baada ya kuumia katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.
Aidha Dickson Job atakosekana kwa takriban mwezi mmoja ndani ya uwanja akiuguza pamoja na kupatiwa huduma za kiafya kutokana na majeraha yake aliyoyapata.
