WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amesema thamani ya mauzo ya bidhaa nje ya nchi yaliongezeka na kufikia dola za Marekani milioni 10,080.9 (bilioni 10.08), kutoka dola milioni 8,702.0 ( bilioni 8.70) mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.
Akiwasilisha hotuba yake bungeni, amesema mafanikio hayo yametokana na kuimarika kwa mazingira ya biashara, upatikanaji wa masoko mapya pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa zenye ushindani katika soko la kimataifa.
Amebainisha kuwa bidhaa zinazoongoza kuuzwa nje ni mazao ya kilimo na madini, huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha sekta ya viwanda na biashara ili kuongeza zaidi thamani ya mauzo ya nje na kuchochea ukuaji wa uchumi.
