Kiungo wa Arsenal, Declan Rice, amejiondoa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England (Three Lions) kinachojiandaa na michezo ya kimataifa ya UEFA Nations League inayotarajiwa kuanza wiki hii.
Kiungo huyo amechukua uamuzi huo ili kupunguza uchovu wa mwili na kuuguza majeraha madogo madogo, lengo likiwa ni kupata muda wa kupumzika baada ya kukabiliwa na ratiba ngumu ya mechi mfululizo za klabu na timu ya taifa.

England itashuka dimbani kumenyana na Hispania Septemba 26, 2026, kabla ya kusafiri kuwafuata Jamhuri ya Czech Septemba 29, 2026.
Baada ya hapo, miamba hiyo itacheza mechi ya tatu dhidi ya Croatia Oktoba 3, 2026, na kuhitimisha mzunguko huo kwa kurudiana na Jamhuri ya Czech nyumbani Oktoba 6, 2026.
