Asma Ahmed- Ngara, Kagera.
NGARA: Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ,imewataka wananchi wanaojihusisha na shughuli za majini wilayani Ngara mkoani Kagera kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El Niño, kufuatilia taarifa iliyotplewa na mamlaka ya hali ya hewa TMA.
Wakitoa elimu juu ya namna ya kuchukua tahadhari hiyo katika kivuko cha MV Ruvuvu kilichopo kata ya Rusumo wilayani humo Afisa Mfawidhi Nahodha Mzee Ally Na Saidi Ahmed Meneja uhusiano na masoko kutoka TASAC Mkoa Wa Kagera wamesema ni vyema kuepuka safari zisizo na ulazima wanapoona mabadiliko ya hali ya hewa.
Aidha, wamesisitiza umuhimu wa kuzingatia maelekezo ya wataalamu, kuhakikisha vyombo vya majini vina vifaa muhimu vya kujiokoa wawapo majini na kutoa taarifa mapema pale wanapoona hatari.
Badhi ya wananchi akiwemo Justine Jacob na Kapteni Odeth Aporinary wamesema elimu hiyo imewasaidia kuelewa namna ya kujilinda dhidi ya madhara ya mvua za El Niño, huku wakiahidi kuzingatia tahadhari hizo.
