Wananchi wa maeneo ya Segese, Lunguya na Kakola wanatarajia kuondokana na adha ya muda mrefu ya vumbi na ubovu wa barabara kufuatia ujenzi wa barabara ya Kahama – Kakola kwa kiwango cha lami.
Mradi huo wenye urefu wa kilomita 73 unaendelea na umefikia zaidi ya asilimia 70 ya utekelezaji huku ukiwa unagharimu shilingi bilioni 101.2
Kamati ya siasa ya CCM Kahama iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga imeeleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo huku ikiwata wahusika kuhakikisha kazi inakamilika kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika.

Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mabula Magangila, amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutasaidia kupunguza changamoto za usafiri na kuondoa hasara zilizokuwa zikiwakumba wafanyabiashara na wasafirishaji kutokana na hali mbaya ya barabara ya awali.
Aidha, ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma katika mikoa ya Shinyanga na Geita.


Hongereni kahama kwa kuboreshewa miundombinu mungu aiongoze serikali itengeneze barabara ya ngara kuja mugoma ina changamoto sana