Bandari ya Kigoma inaendelea kufanyiwa maboresho makubwa kupitia uwekezaji wa shilingi bilioni 76 unaojumuisha ujenzi wa gati jipya la abiria, jengo la kisasa la huduma na barabara za kisasa za kuingia na kutoka bandarini sambamba na ukarabati mkubwa wa meli kongwe ya MV Liemba.

Akizungumza baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya miradi hiyo, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema maboresho ya miundombinu hiyo kutaongeza ufanisi wa huduma za usafirishaji, kukuza biashara na kuinua kipato cha wananchi wa ukanda wa Ziwa Tanganyika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli (TASHICO), Eric Hamissi, amesema ukarabati wa MV Liemba ambao utakamilika mwezi Julai mwaka huu utasaidia kumaliza changamoto ya usafiri katika mwambao wa Ziwa Tanganyika.
