Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema kuwa mazingira yana umuhimu mkubwa katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa taifa, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhimilivu wa ongezeko la watu Duniani.
Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani leo Dkt. Nchimbi, amesema kuwa kwa sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu takriban Milioni 67 ambapo idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia watu Milioni 118 ifikapo mwaka 2050.
Ameongeza kuwa, ongezeko hilo la watu litahitaji uwepo wa rasilimali nyingi muhimu zinazotegemea mazingira yaliyo bora, kama vile maji, chakula, ardhi yenye rutuba, makazi, nishati na mifumo ya huduma za jamii.
Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo Dira 2050 tuwajibike kukijanisha Tanzania.
