Na William Mpanju- Biharamulo, Kagera
Mahakama ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera imemhukumu mkazi wa kitongoji cha Mishoroti kata ya Nyakahura wilaya ya Biharamulo, kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa ke wa kambo mwenye umri wa miaka 10.
Akitoa hukumu hiyo ,hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Biharamulo Frola Ndale mbele ya mwendesha mashitaka wakili wa serikali Salvatory Benedicti amemtaja mshitakiwa kuwa ni Ngika Ngusa mwenye umri wa miaka 56 mkazi wa Nyakahura.
Kabla ya hukumu hiyo ,Hakimu Ndale amesema Ngika Ngusa mwenye umri wa miaka 56 alitenda kosa la kumbaka mtoto wake wa kambu akiwa na miaka 10 tangu May 01, 2015 hadi mwezi june 2024 hadi kumzalisha watoto wawili,
Amesema baada ya mahakama kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili kupitia vipimo vya madaktari mahakama imeridhika na ushahidi wa upande wa jamhuri bila kuacha shaka dhidi ya mshitakiwa Ngika Ngusa hivyo anastahili kutumikia kifungo cha miaka 30 jera.
.Awali wakili wa serikali Salvatory Benedicti ameiomba mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo kwa kuwa vitendo vya ubakaji vimekidhiri katika wilaya ya Biharamulo.
