Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC, limeandaa kwa mara ya kwanza Kongamano la Makatekista Kitaifa, linalofanyika Jimbo la Singida kuanzia Septemba 7 hadi 11 mwaka 2026.
Kongamano hilo linafanyika chini ya kauli mbiu, “Nimtume nani? Mimi hapa, nitume,” kutoka kitabu cha Isaya 6:8.
Katekista ni mwamini mlei anayesaidia Kanisa kufundisha na kurithisha imani kwa waamini. Pia hushiriki katika uinjilishaji, kuwaandaa waamini kupokea Sakramenti na kuwasaidia kuelewa mafundisho ya Kanisa.
Kupitia kongamano hilo, Makatekista wanahimizwa kuwa waaminifu katika maisha na utume wao, huku wakifuata mafundisho, Mapokeo na uongozi wa Kanisa.
Kilele cha kongamano hilo kinatarajiwa kuwa Septemba 10, kwa Ibada ya Misa Takatifu na sherehe za Makatekista katika Viwanja vya Askofu Mabula, Singida.
