Siku za Vijana wa Afrika Magharibi, JOAJ, za mwaka 2026 zimefunguliwa Septemba 7 jijini Accra, Ghana, zikihusisha Vijana Wakatoliki kutoka nchi 16 za Afrika Magharibi.
Vijana hao wanakutana kwa siku tano kujadili nafasi yao katika kujenga amani na matumaini, chini ya kauli mbiu, “Jipe moyo: Vijana Wakatoliki, watendaji na mawakala wa amani na matumaini ya Afrika Magharibi.”
Miongoni mwa mada zitakazojadiliwa ni uinjilishaji kupitia mitandao ya kijamii, uongozi wa vijana, mabadiliko ya kijamii, ujenzi wa amani, mabadiliko ya tabianchi na mapambano dhidi ya ugaidi na migogoro.
Aidha, vijana watashiriki hija, katekesi, Ibada za Misa Takatifu pamoja na shughuli za kitamaduni.
Siku hizo zinatarajiwa kuhitimishwa Septemba 11, ambapo vijana watatumwa kurejea katika nchi zao wakiwa na jukumu la kuwa mabalozi wa amani, matumaini na maridhiano.
