Baba Mtakatifu Leo XIV anatarajiwa kufanya ziara ya kichungaji katika San Marino mnamo Agosti 22, 2026, ikiwa ni sehemu ya ratiba yake ya ziara nchini Italia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Nyumba ya Kipapa, ziara hiyo itafanyika baada ya Papa kukubali mwaliko wa Makapteni Wakuu wa San Marino, Matteo Rossi na Lorenzo Bugli. Papa atatembelea taifa hilo dogo asubuhi ya siku hiyo kabla ya kuendelea na ratiba nyingine.
Aidha, alasiri ya Agosti 22, Papa Leo XIV ataelekea katika Rimini kushiriki katika Mkutano wa Watu, maarufu kama Meeting di Rimini, tukio linalowakutanisha viongozi wa dini, siasa, utamaduni na jamii kwa ajili ya mijadala kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii na kiroho.
Ziara hiyo inaonesha dhamira ya Baba Mtakatifu ya kuendelea kuwa karibu na waamini pamoja na jamii mbalimbali, huku akihimiza mshikamano, mazungumzo na kukuza maadili ya kiroho katika jamii za kisasa.
