Tanzania inatarajia kuanzisha Taasisi ya Taifa ya Teknolojia ya Kidijitali katika eneo la Nala, Dodoma, kwa lengo la kuwajengea Watanzania ujuzi wa kutumia teknolojia zinazoibuka.
kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Angellah Kairuki akiwa nchini Korea Kusini , kuwa taasisi hiyo itatoa mafunzo katika maeneo ya Akili Unde (AI), roboti, Intaneti ya Vitu (IoT) pamoja na teknolojia nyingine za kisasa.
Waziri Kairuki amesema uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Korea Kusini, ulioanza mwaka 1992, umeendelea kutoa fursa za ushirikiano katika teknolojia, ubunifu na maendeleo ya rasilimali watu.
Amesema Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Korea na Afrika wa Ushirikiano wa Kiuchumi (KOAFEC), unaofanyika Seoul kuanzia tarehe 8 hadi 11 Septemba 2026, ni jukwaa muhimu kwa Tanzania kuonesha miradi yake ya maendeleo, kutangaza fursa za uwekezaji na kuvutia wawekezaji zaidi katika miradi ya maendeleo nchini.

katika picha ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Angellah Kairuki
Bofya hapo chini kusikiliza sauti
