Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo amesema Kampuni ya Perenco Group ipo katika hatua za mwisho kuwekeza zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 300 katika mradi wa uzalishaji umeme kupitia mfumo wa upepo Mkoani Singida.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiriano wa Afrika Mashariki, leo Mei 26, 2026 Bungeni Jijini Dodoma, Waziri Kombo amesema mradi huo utaongeza Megawati 200 katika Gridi ya Taifa ya Umeme na kuchangia upatikanaji wa Nishati safi Nchini.
anasema “Miongoni mwa Taasisi zenye nia ya kuwekeza Nchini ni SinoAm LLC ambayo imeonesha nia ya kuwekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni Tano katika Sekta ya Miundombinu ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR) pia katika Ushoroba wa Mtwara, Bandari ya Mtwara na Barabara ya Dar – Morogoro Expressway kupitia mfumo wa Ushirikiano wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPP)”.

Picha ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo akiwa bungeni Dodoma leo may 26,2026
