Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman amesema chama hicho kiko tayari kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar, baada ya kukamilika mchakato wa kamati ya pamoja kati yake na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Othman amesema hayo leo, Septemba 8, 2026, wakati akifungua mjadala katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini, Uchaguzi Mkuu wa 2025 na Mustakabali wa Taifa.
Amesema ACT-Wazalendo na CCM wamekubaliana kuunda kamati ya pamoja yenye wajumbe watano kutoka kila upande, itakayoshughulikia maeneo yaliyokubaliwa na vyama hivyo.
Kwa mujibu wa Othman, kamati hiyo inatarajiwa kuzinduliwa kabla ya kuisha Septemba 2026 na itafanya kazi kwa kuzingatia hadidu rejea zilizokubaliwa na pande hizo.
βTumekubaliana baada ya kuiunda Kamati ya Pamoja na kuizindua, sisi ACT-Wazalendo tumekubaliana tutaingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Mchakato wake umeshaanza na tunaamini katika baraza lijalo la Wawakilishi huenda wataapishwa,β amesema.
