Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Kardinal Protase Rugambwa amesema Serikali imeendelea kuunga mkono juhudi za Kanisa Katoliki katika kujenga jamii yenye maadili mema, mshikamano na maendeleo bila mafarakano.
Kardinali Rugambwa amesema hayo wakati wa harambee maalumu ya kuchangia fedha za umaliziaji wa ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Bernadetha wilayani Nzega, iliyofanyika chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paulo Chacha.
Katika harambee hiyo, wadau mbalimbali pamoja na viongozi wa kitaifa walichangia zaidi ya shilingi milioni 200, kiasi kinachofikia zaidi ya asilimia 60 ya fedha zinazohitajika kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo.
Amina Deogratius Semagogwa (SEMA G)
ni mwandishi wa habari na mtangazaji mahiri wa Radio mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika tasnia ya habari, Amebobea katika kuandaa na kuendesha vipindi vyenye uzito vinavyolenga kuibua mijadala ya kijamii, hususan katika malezi bora ya watoto na masuala ya utawala bora.
Kupitia kalamu na sauti yake Amina ametunukiwa tuzo zaidi ya 10 za uandishi bora wa habari nchini Tanzania , Amina amejijengea nafasi ya kuwa daraja kati ya jamii na maarifa, akiamini kuwa uandishi wa habari si kuripoti tu bali ni chombo cha kuelimisha, kuhamasisha na kuleta mabadiliko chanya, Ana mtindo wa kipekee unaochanganya weledi, uchambuzi na uwasilishaji unaogusa maisha halisi ya watu.
Kauli mbiu: Sauti ya jamii, dira ya mabadiliko.